Africa

Onana astaafu Cameroon

GOLIKIPA Andre Onana amestaafu kucheza timu ya soka ya taifa ya Cameroon baada ya kutoelewana na Kocha Mkuu Rigobert Song wakati wa michuano ya Kombe la Dunia 2022 iliyofanyika Qatar.

Kocha Mkuu wa Cameroon, Rigobert Song.

Song alisema Onana aliomba kutocheza mechi ya pili hatua ya makundi dhidi ya Serbia.

Baada ya hali hiyo Onana alisimamishwa timu ya taifa na hakucheza tena hivyo aliondoka Qatar.

Onana mwenye umri wa miaka 26 amesema leo kuwa ” habari zake timu ya taifa ya Cameroon zimefika mwisho.”

“Wachezaji huja na kuondoka, majina ni ya kupita muda mfupi, lakini Cameroon huja kabla ya mchezaji au mtu yeyote,” amesema mchezaji huyo wa Inter Milan.

Onana aliitwa kwa mara ya kwanza timu ya taifa 2016 akicheza mechi 34.

Cameroon iliyokuwa kundi G Kombe la Dunia pamoja na Brazil, Serbia na Uswisi iliondolewa hatua ya makundi.

Related Articles

Back to top button