Ofisi ya Mama mkwe wa Jux yateketea kwa moto

LAGOS: TUKIO la moto katika ofisi ya muigizaji wa kike wa Nigeria na mama mkwe wa msanii wa Tanzania Juma Jux, Iyabo Ojo limetokea kwa moto usiku wa jana Julai 8, 2025 majira ya saa saba huko Lagos nchini Nigeria.
Kisa hicho kimetokea miezi miwili tu baada ya harusi ya binti wa mama huyo, Priscilla Ojo na mwimbaji maarufu wa Tanzania, Juma Jux.
Akishiriki video ya tukio hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram, muigizaji huyo amesema hakuna mtu aliyepata madhara yoyote zaidia ya ofisi yake yote kuteketea na moto.

Kisa hicho cha kusikitisha kilitokea katika Jimbo la Lagos mnamo Jumanne usiku mwendo wa saa saba usiku.
“Hii imetokea leo usiku mwendo wa saa 7, Ofisi yangu ilishika moto. “Shukrani kwa huduma ya Zimamoto ya Nigeria na wafanyakazi wangu kwa kuokoa kile kilichosalia. Tunashukuru, hakuna maisha yaliyopotea. Ibilisi alitujaribu lakini Mungu alisema hapana. Mungu akiwa upande wangu, tutarudi na ubora zaidi”, amesema.




