La Liga

Njiwa wa Habari njema atua Barca

BARCELONA, Wababe wa soka nchini Hispania FC Barcelona wamethibitisha kurejea kwa beki wao wa kati Andreas Christensen baada ya raia huyo wa Denmark kufaulu vipimo na kupata ruhusa kurejea uwanjani kutoka kwa madktari wa timu hiyo kufuatia kukosekana tangu mwisho wa Januari Mwaka huu.

Christensen mwenye miaka 28 alipata majeraha kwenye ‘kigimbi’ cha mguu wake wa kulia lakini sasa madaktari wa klabu hiyo wamemuwashia taa ya kijani kocha Hansi Flick kumtumia tena beki huyo hata katika mchezo ujao dhidi ya Real Sociedad siku ya Jumapili.

Kuruhisiwa kwa Christensen kunasitisha masaibu ya beki huyo kukosa mechi 7 za mashindano yote ikiwemo dhidi ya Atalanta kwenye Ligi ya Mabingwa, michezo ya Laliga dhidi ya Alaves, Sevilla, Rayo Vallecano, na Las Palmas na zile za Copa del Rey dhidi ya Valencia na Atletico Madrid.

Haujawa msimu mzuri kwa Christensen baada ya kuandamwa sana na majeraha akicheza dakika 26 pekee msimu huu katika mchezo dhidi ya Valencia mapema mwezi Agosti na baadaye mwezi huo kuchanika mishipa ya Achilles kwenye mguu wake wa kulia, jeraha lililomuweka nje ya uwanja kwa miezi minne.

Baadaye Januari 18 alikuwemo kwenye kikosi kilichotajwa kukipiga dhidi ya Getafe lakini hakugusa nyasi za uwanja. Alikuwa pia miongoni mwa majina yaliyotajwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Benfica na ule wa Laliga dhidi ya Valencia ambazo hakucheza, na sasa kocha Flick anasema kurejea kwake ni masaada mkubwa.

Related Articles

Back to top button