Africa

Nilikaribia kumsajili Mayele-Marchand

KOCHA Mkuu wa Club Africain ya Tunisia, Bertrand Marchand amesema anatarajia upinzani mkali kutoka kwa wenyeji wao Yanga katika mchezo wa kufuzu makundi Kombe la Shirikisho Afrika Novemba 2 lakini wamejipanga kuhakikisha hawaondoki patupu.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari Dar es Salaam leo kocha huyo amesema wamekuja kwa tahadhari kubwa wakifahanu fika ubora wa timu wanayokwenda kukutana nayo lakini watajitahidi kuhakikisha wanakabiliana na lolote litakalo tokea.

“Yanga ni klabu kubwa Afrika ina kocha mzuri lakini pia wachezaji bora kwenye ukanda huu na mfahamu Tuisila Kisinda, Fiston Mayele na hata Jesus Moloko ni wachezaji ambao walifanya vizuri pale AS Vita kuna kipindi nilikaribia kumsajili Mayele kabla ya kuwahiwa na Yanga,” amesema kocha huyo.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo wa Noveemba 2 na nia ni kurudisha furaha kwa mashabiki wa klabu.

Nabi amesema hawezi kuzungumzia wapinzani wao bali kitu cha msingi ni kuona ni namna gani wanashinda mechi hiyo.

“Tulifanga makosa kwenye mchezo wa nyumbani dhidi ya Al Hilal safari hii hatupo tayari kurudia makosa tumejipanga kuhakikisha mchezo huu tunaumaliza hapa nyumbani,amesema Nabi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button