
ROBO fainali ya mwisho ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) inapigwa leo kati ya Yanga na Geita Gold kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Geita Gold itataka kulipiza kisasi cha kuchapwa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara timu hizo zilipokutana mara ya mwisho Mach 12, 2023.
Timu zilizofuzu kucheza nusu fainali ya ASFC ni Simba, Azam na Singida Big Stars.