Kikapu
Ni vita ya Jokic, Lebron fainali NBA

BAADA ya kunyukwa mchezo wa fainali ya kwanza Ligi ya NBA, Los Angeles Lakers kesho saa 9:30 ( usiku wa leo kuamkia kesho) watakuwa ugenini kuwavaa Denver Nuggets katika fainali ya pili Ukanda wa Magharibi.
Nuggets wataingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa pointi 132-126 katika mchezo wa kwanza.
Lakers wamefika hatua hiyo baada ya kuifunga Golden State Warriors pointi 122-101, huku Lebron James akiibuka MVP wa mchezo kwa kupiga pointi 30, assist na rebound 9 katika dakika 43 alizocheza.
Nuggents walifika fainali baada ya ushindi wa pointi 125-100 dhidi ya Phoenix Suns katika mchezo wa nusu fainali.