Kikapu

Boston Celtics yatinga fainali NBA

KLABU ya Boston Celtics itacheza fainali ya michuano ya NBA, Marekani baada ya kushinda mfululizo wa nusu fainali ya Eastern Conference dhidi ya Indiana Pacers.

Katika mchezo wa nusu fainali Jaylen Brown alimpasia mpira Derrick White aliyepata alama 3 muhimu huku zikiwa imesalia sekunde 45 mchezo kumalizika na Cletics kuibuka na ushindi wa 105-102.

Hiyo ni mara ya pili Celtics kutinga fainali za NBA katika misimu 3.

“Tuna kundi la watu bora kwenye chumba hiki cha kubadilishia nguo, watu wa nguvu. Walimu wetu wamekuwa bora na sasa tunaelekea hatua inayofuata,” amesema Brown.

Kocha wa Celtics Joe Mazzulla amewasifu wachezaji wake akisema ni wasikivu na wenye kujituma.

Related Articles

Back to top button