World Cup
		
	
	
Ni mtoano 16 bora Kombe la Dunia
						Mechi za mtoano timu 16 bora katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea Qatar zinaanza leo kwa michezo miwili.
Mchezo wa kwanza utazikutanisha Uholanzi na Marekani wakati mchezo utakaofuata utakuwa kati ya Argentina na Australia.
Timu mbili tu za Afrika zilizosalia ambazo ni Senegal itakayopambana na England Desemba 4 wakati Morocco itakuwa dimbani Desemba 6 kuvaana na Hispania.
Cameroon, Ghana na Tunisia tayari zimetolewa katika hatua ya makundi.
				
					



