Kwingineko
Ni Barca au Osasuna fainali Super Cup?
NUSU fainali ya pili ya Super Cup Hispania kati ya Barcelona na Osasuna inapigwa leo Saudi Arabia.
Mshindi wa mchezo huo kwenye uwanja wa Awwal Park , jijini Riyadh atacheza fainali dhidi ya Real Madrid ambayo imeitoa Atletico Madrid kwa mabao 5-3.
Bingwa mtetezi wa Super Cup ya Hispania ni Barcelona baada ya kuifunga Real Madrid mabao 3-1 Januari 15, 2023.




