EPL

Ndoa ya Tuanzebe, United yafika mwisho

UNAWEZA kusema ndoa imevunjika kati ya Manchester United na Alex Tuanzebe baada ya kuthibitika kuwa beki huyo raia wa England hatokuwa sehemu ya kikosi hicho msimu wa 2023/2024.

Tuanzebe ,25, mzaliwa wa Bunia, nchini DR Congo, tangu mwaka 2015 hajawahi kupewa mkataba na timu yoyote zaidi ya kutolewa kwa mkopo katika timu za Aston Villa mara tatu, Napoli na sasa anakipiga Stoke City kwa mkopo.

Mkataba wa beki huyo unaisha msimu huu Man United haina mpango wa kumuongezea hivyo ataondoka kama mchezaji huru kwenda anapopataka.

Tuanzebe alijiunga na United 2015 akitokea kikosi cha vijana cha timu hiyo, aliitumikia United misimu mitatu ambapo mwaka 2018 alitolewa kwa mkopo kwenda Aston Villa.

Tuanzebe hajawahi kufunga bao kwenye maisha yake ya soka.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button