Nabi hajaridhishwa na matokeo

KOCHA wa Yanga, Nasredden Nabi amesema hajaridhishwa na matokeo ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallant kwenye nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Kocha Nabi anasema licha ya ubora wa wapinzani wao lakini kipindi cha kwanza timu yake haikucheza vizuri hivyo kuufanya mchezo kuwa mgumu.
“wachezaji wangu hawakufanyia kazi yale niliyowaelekeza ndio maana sijaridhishwa na matokeo haya”
“Wachezaji wanapaswa kutimiza majukumu yao kwa ufanisi ili tufuzu, kwa sasa bado hatujafuzu tuna kazi ya kufanya kwenye mchezo wa mkondo wa pili nchini Afrika kusini.”
Kwa upande wake kocha wa Marumo Gallants Dylan Kerr Yeye amelia na safu ya ushambuliaji ya timu yake kwa kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza.
“Tumekosa nafasi nyingi sana nafasi kama nne za wazi,
” tulishindwa kutumia vyema nafasi tulizotengeneza japo inatokea katika soka mara nyingi tuu kwenye soka tutayafanyia kazi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili tukiwa nyumbani”
Magoli ya Yanga kwenye mchezo huo yamefungwa na Stephan Azizi ki dakika ya 64 huku Bernad Morrison akipigilia msumari wa mwisho dakika ya 90+2 ya mchezo, na sasa Yanga wanasubiri mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa Afrika kusini Mei 17 mwaka huu.