Habari Mpya

Nabi azipigia hesabu Ruvu, Al Hilal

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema baada ya kumalizana na Zalan, nguvu na akili zake amezielekeza kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting na baada ya hapo ataanza kuufanyia kazi mchezo dhidi ya Al Hilal.

Akizungumza na Spotileo kocha huyo amesema siku 10 zinamtosha kukiandaa kikosi chake kuikabili Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Oktoba 8 uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

“Tuna siku 10 kabla ya kuikabili Al Hilal lakini kabla ya mchezo huo tutacheza na Ruvu Shooting mchezo wa ligi ni mechi nzuri ambayo itatupima kabla ya kuwakabili wasudan,” amesema Nabi.

Kikosi cha Yanga kilichanza katika mchezo dhidi ya Zalan ya Sudan Kusini katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Septemba 17, 2022.

Amesema kwa sasa wachezaji wanafanya mazoezi ya kwenda na kurudi nyumbani na wiki moja kabla ya mchezo wa Ruvu wataingia kambini na hawatatoka mpaka watakapocheza na Al Hilal.

Nabi amesema kwa maandalizi wanayoyafanya hivi sasa matumaini ya kucheza hatua ya makundi msimu huu ni makubwa na amewataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwapa sapoti.

Yanga itacheza dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi Oktoba 3.

Related Articles

Back to top button