Ligi KuuNyumbani

Nabi ataka ushindi Yanga uendelee

KOCHA wa Yanga, Nasriddine Nabi amesitisha mapumziko ya wachezaji wa timu hiyo na kuwaita kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City Novemba 26 uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na SpotiLeo, kocha huyo amesema baada ya kuangalia mchezo wa Simba na Mbeya City amebaini uzito wa mechi hiyo ili kujiandaa kwa ajili ya mchezo huo.

“Mbeya City ni timu ngumu tunahitaji kuupa uzito wa kipekee mchezo huo ikiwemo kufanya maandalizi mazito kuhakikisha tunashinda na kuendeleza rekodi yetu nzuri ya ushindi,” amesema Nabi.

Nabi amesema pamoja na uchovu wa wachezaji wa kikos chake, kupata siku mbili za mazoezi anaamini zitawajenga na kuwasaidia wachezaji kuendana na kasi ya mchezo.

Yanga inaongoza katika msimamo wa Ligi kuu ikikusanya pointi 29 baada ya michezo 11.

Related Articles

Back to top button