Mwanaume wa kwanza mbunifu mweusi Kushinda Tuzo ya Oscar

HOLLYWOOD: MBUNIFU wa mavazi mwenye umri wa miaka 60, Paul Tazewell Amekuwa mwanaume wa kwanza mweusi kutwaa tuzo ya Ubunifu Bora wa Mavazi aliyoifanya katika filamu ya ‘Wicked’.
Akizungumza kwenye jukwaa katika ukumbi wa michezo wa Dolby wa Los Angeles, alisema: “Hii inashangaza kabisa. Asante, Academy, kwa heshima hii muhimu. Mimi ndiye mtu mweusi wa kwanza kupokea tuzo ya ubunifu wa mavazi kwa kazi yangu katika filamu ya ‘Wicked’. Ninajivunia sana kwa hili.”
Paul ambaye aliteuliwa katika kitengo cha ‘West Side Stori’ mnamo 2022 aliendelea kuwashukuru Cynthia Erivo na Ariana Grande, pamoja na wasanii wengine katika filamu ya ‘Wicked’.
Ushindi wa Paul ulikuja katika kitengo ambacho pia kilimshirikisha Arianne Phillips, Janty Yates na David Crossman ‘Gladiator II’, Lisy Christl ‘Conclave’ na Linda Muir ‘Nosforatu’.
Ruth E. Carter pia ndiye alikuwa mwanamke wa kwanza Mweusi kushinda Ubunifu Bora wa Mavazi kupitia filamu ya ‘Black Panther’ ya mwaka 2018 na alirudia pia katika muendelezo wa filamu ya 2022 ‘Black Panther: Wakanda Forever’.
Paul ameshinda tuzo hiyo msimu huu wa tuzo kwa kazi yake ya kuunda zaidi ya mavazi 1,000 katika filamu hiyo ya ‘Wicked’, akishinda katika tuzo za BAFTAS, Chaguo la Wakosoaji na Chama cha Wabunifu wa Mavazi.
Ushindi huu wa Tuzo la Academy unamweka Paul kwenye robo tatu kwenye njia ya EGOT inayotamaniwa zaidi, baada ya kushinda Emmy ya ‘The Wiz Live’ na Tuzo ya Tony ya ‘Hamilton’. Pamoja na Oscar, EGOT inazungushwa na ushindi wa Grammy.




