Ligi KuuNyumbani

Mwambusi kaifunga Yanga lakini hana furaha

KOCHA Mkuu wa Ihefu Juma Mwambusi amesema pamoja na kuifunga Yanga lakini yeye na wachezaji wake wana kazi ya kufanya kuiondoa timu hiyo kwenye nafasi mbaya iliyopo kwenye msimamo wa Lig Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na SpotiLeo kocha huyo amesema amempangia kila mchezaji majukumu maalumu kitu ambacho anaamini kitawasaidia kupata matokeo mazuri.

“Ninachotaka kila mchezaji atimize majukumu yake kwa asilimia 70 kinyume na hapo hatutaelewana na mchezaji asiyefikia malengp,” amesema Mwambusi.

Amesema anatambua kuwa haitakuwa rahisi lakini kwa ushindani uliopo na nafasi Ihefu iliyopo kwenye ligi hakuna namna lazima kupangiana mikakati ili kujinasua kwenye janga la kushuka daraja.

Desemba 2 Ihefu itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Kagera Sugar mchezo unaotarajiwa kuchezwa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ihefu inashika nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 14.

Related Articles

Back to top button