Masumbwi

Mwakyembe ‘atandikwa’  Urusi

URUSI: BONDIA wa ngumi za kulipwa Tanzania,  Emmanuel Mwakyembe ampoteza  pambano lake dhidi ya mwenyeji wake Tigran Uzlyan, nchini Urusi.

Mwakyembe amepoteza pambano hilo la raundi 10 lilofanyika Jumatano Usiku , Januari 22 nchini Urusi.

Bondia huyo mwenye ana hadhi ya nyota mbili akiwa na rekodi ya kucheza mapambano 16 akishinda 12 matatu kwa ‘KO’, kupoteza mawili na kutoka sare mawili.

Mwakyembe anashika nafasi ya 152 katika ubora wa mabondia 2,503 Duniani huku Tanzania akiwa namba nne kati ya 115 kwa uzito wa Light.

Kabla ya kupoteza pambano la Urusi, mara ya mwisho  Mwakyembe alipoteza pambano Agosti 14, 2020 alipopigwa na Juma Choki kwa ‘points’ za majaji wote watatu kwenye pambano lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.

Kwa mpinzani wake, Uzlyan mwenye nyota tatu amecheza mapambano 11, kushinda 10 na sita kati ya hao kwa ‘KO’, amepoteza moja kwa pointi.

Uzlyan anashika nafasi ya 50 kati ya mabondia 2,503 Duniani na yupo nafasi ya tatu katika ubora wa nchini kwao kati ya mabondia 33.

Related Articles

Back to top button