Muigizaji Vibhu Raghave afariki jana, kuzikwa

MUMBAI:MUIGIZAJI wa michezo ya runingani Vibhu Raghave, anayejulikana kupitia filamu ya ‘Nisha Aur Uske Cousins’, amezikwa leo huko Mumbai baada ya kufariki dunia jana kutokana na kuugua saratani ya utumbo mpana kwa muda mrefu.
Jina lake halisi ni Vaibhav Kumar Singh Raghave, amefariki jana Juni 2, 2025 katika Hospitali ya Nanavati huko Mumbai ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.
Vibhu aligunduliwa kuwa na saratani ya utumbo mpana mwaka wa 2022. Marafiki zake wa karibu, akiwemo Addite Malik na Saumya Tandon, walithibitisha habari za kifo chake kwa kushiriki shughuli za mazishi yake ambayo yanafanyika leo Juni 3, 2025.
Addite aliandika: “Nafsi safi zaidi, mwanga wa nguvu & chanya. Tabasamu lake lingeweza kuangaza chumba chochote na uwepo wake pekee ulifanya kila kitu kihisi vizuri zaidi. Alikabiliana na maisha kwa neema isiyo na kifani na kuacha upendo ambao hautafifia kamwe. Atakumbukwa Daima”.