Featured
Mteleza kwenye barafu afariki dunia
MCHEZAJI wa kuteleza kwenye barafu wa Italia Elena Fanchini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 37 baada ya vita dhidi ya saratani.
Shirikisho la Michezo ya majira ya baridi la nchi hiyo limetangaza.
“Mwisho wa ugonjwa mbaya, Elena Fanchini amefariki dunia nyumbani kwake Solato,”limesema shirikisho hilo.
Fanchini alishindana kwenye michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi mwaka 2006, 2010, na 2014 lakini alilazimika kujitoa kwenye michezo ya Pyeongchang ya mwaka 2018 alipogundulika kuwa na saratani.
Mchezaji huyo alifanikiwa kushinda medali nne za Kombe la Dunia, akishinda pia medali mbili za dhahabu katika mteremko mnamo 2005 na 2015.




