Msechu aelezea afya yake

Mwimbaji wa Bongo Fleva nchini Peter Msechu, ameeleza maendeleao ya afya yake, katika harakati za kupunguza uzito kwa kuzuia hamu ya kula.
“Anyways kuna watu wanasema sana kwamba nimepoteza muda na pesa miezi sita kupungua kilo 17 sio sawa, wengine wanasema ungefanya diet siku mbili tusijui mazoezi, hivi mnajua ni kwa kiasi watu wenye miili mikubwa wanahangaika kila kukicha kupunguza uzito?.”
“Kazi kubwa kwangu ilikuwa ni kuhakikisha natafuta njia sahihi ya Kuzuia hamu ya kula na kiwango kidogo cha kula Kwa sababu hata iweje kwa akili zangu nisingeweza kufatisha diet at all kwa kuona kilichopo mbele yangu nakitamani na sitakiwi kukila”.
“Sasa hapo ndio puto likawa jawabu langu kwa sababu, hata chakula nikitamani vipi nitakula vijiko vitatu hadi sita nimeshiba, nikilazimisha natapika. Hiyo kwangu ndio ilikuwa njia sahihi ya kuzuia kula”




