EPLKwinginekoSerie A

Mourinho ataka kurejea EPL

KOCHA wa klabu ya Roma ya Italia, Jose Mourinho ana nia ya kurejea Ligi Kuu ya England(EPL0 msimu ujao kufuatia mfadhaiko wa ukosefu wa fedha kutoka uongozi wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti wawakilishi wa Mourinho wamesema atakuwa tayari kurejea Chelsea kwenye nafasi yoyote lakini klabu hiyo imeweka wazi inakusudia kuendelea na Graham Potter.

Mke na watoto wa Murinho bado wako London na kocha huyo siku zote amekuwa akipendelea kufanya kazi EPL kuliko ligi nyingine yoyote.

Mreno huyo ameshinda Europa Conference League akiwa Roma msimu uliopita na sasa klabu hiyo ipo nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu Italia, Serie A lakini ina ukosefu wa fedha kuwa mshindani wa ubingwa.

Nafasi ya ukocha katika Klabu ya West Ham United pia inaweza kupatikana hivi karibuni ikitiliwa maanani David Moyes hana wakati mzuri ingawa Mourinho hawezi kuondoka Roma katikati ya msimu.

Related Articles

Back to top button