Mavazi

Miss Tanzania 2020: Napenda kuvaa nadhifu bila kuacha mwili wazi

DAR ES SALAAM: MISS Tanzania 2020, Rosey Manfere, amesema kuwa katika maisha yake anapenda sana kuvaa vizuri na kupendeza, lakini hapendi kuvaa mavazi yanayoacha mwili wake wazi.

Akizungumza na Spoti Leo kuhusu suala la mavazi, Rosey amesema mtu anaweza kuvaa kwa staha na akaonekana mrembo bila kuacha mwili wazi, kinachohitajika ni kuzingatia aina ya sehemu au tukio analokwenda.

Amesema:
“Napenda kuvaa nguo zinazonitambulisha kwa watu kama mwanadada wa Kitanzania mwenye maadili yote. Si lazima kuvaa nguo za utupu ili kuonekana nadhifu au mzuri.”

Kwa mujibu wa Rosey, mavazi ni sehemu ya utambulisho wa mtu, hivyo ni muhimu kuchagua nguo zinazoakisi heshima, maadili na tamaduni za Mtanzania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button