
KLABU ya Geita Gold Imetangaza kuachana na kocha wake Fred Felix Minziro baada ya kocha huyo kumaliza mkataba wake na kuomba kuondoka klabuni hapo.
Taarifa iliyolotewa na Geita Gold leo Juni 20 imeeleza kuwa Minziro ameomba kutoongeza mkataba ili akatafute changamoto nyingine.
Kocha huyo ndiye aliyeipandisha Geita Gold ligi kuu na kuisadia kumaliza nafasi nne za juu kwenye msimu wake wa kwanza ligi kuu na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya shirikisho barani Afrika.
Geita Gold imewaondoa shaka mashabiki wa timu hiyo kuwa itatangaza benchi jipya la ufundi mchakato utakapokamilika.



