Muziki
Mimi ni msanii bora wa Singeli-D Voice

DAE ES SALAAM:Msanii wa kizazi kipya Dennis Mwasele, maarufu kama D Voice kutoka lebo ya Wasafi, amesema kwa sasa ndiye msanii namba moja kwenye muziki wa Singeli.
D Voice alizungumza hayo katika mahojiano na Wasafi Fm, akionesha furaha kwa mafanikio aliyoyapata chini ya lebo ya Wasafi.Alisisitiza kuwa juhudi zake na usimamizi wa lebo hiyo vimechangia safari yake ya mafanikio.
D Voice amesema anaongoza kwa kuwa na nyimbo zinazofanya vizuri zaidi, anakubalika zaidi kwa mashabiki, anaongoza kwa idadi ya wafuasi mitandaoni, na pia ndiye msanii mdogo anayelipwa zaidi kwa sasa.
Ni ngoma gani ya D Voice inayokuvutia zaidi?




