Tetesi

Miamba mitatu Ulaya yamwania Rashford

AKIWA amepoteza umuhimu wake Manchester United, fowadi Marcus Rashford ameibuka kuwa mlengwa wa uhamisho kwenda Barcelona, Paris Saint-Germain and Juventus huku timu zote tatu tayari zinaandaa maombi ya umsajili. (Fichajes)

Nyota mwingine anayepambana beki wa kati Raphael Varane, amehusishwa na uwezekano wa kurejea Real Madrid kuchukua nafasi ya majeruhi David Alaba.(Bild)

Lakini Kocha Erik ten Hag anataka kumbakisha Varane katika klabu ya United zaidi ya Januari pamoja na kiungo Casemiro.(ESPN)

Arsenal ipo mbele ya Chelsea katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney, ambaye ana nia kuijunga na The Gunners.(Independent)

Liverpool inataka winga wa Bayern Munich Leroy Sane awe mbadala wa Mohamed Salah, ambaye anaweza kuuzwa majira yajayo ya kiangazi wakati atakapofikia miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake. (Fichajes)

Pia kuna uwezekano kiungo wa Inter Nicolo Barella akasaijiliwa Liverpool ingawa Chelsea pia ina nia na mtaliano huyo.(Fichajes)

Manchester United imejiunga na Tottenham Hotspur na West Ham United katika kusaka saini ya kiungo wa Chelsea Conor Gallagher.(TEAMtalk)

Lakini Chelsea imeamua kuzuia mipongo yoyote kutoka Tottenham kwa kuwa haitaki kuzidisha upinzani wa moja kwa moja.(Football Insider)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button