Featured

Messi kurejea Barca msimu ujao

Messi akionekana mwenye huzuni wakati akizungumza na vyombo vya habari na wachezaji wenzake makao makuu ya Barcelona Nou Camp kabla ya kuondoka.

MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain atarejea Barcelona majira yajayo ya joto baada ya kumaliza tofauti na Rais wa Barca.

Mshindi huyo mara 7 wa tuzo ya Ballon d’Or alijiunga na PSG baada ya Barca kutoa taarifa ikisema anaondoka Hispania kutokana na masharti ya kifedha yaliyowekwa dhidi ya klabu hiyo na Shiriksho la Soka-La Liga.

Hata hivyo, ripoti zimesema Messi aliyejiunga na PSG mwaka 2021 atarejea Barcelona Julai Mosi, 2023 wakati mkataba wake utakapokwisha makao makuu ya Ufaransa majira yajayo ya joto.

Rais wa Barcelona, Joan Laporta.

Inaaminika Messi atarejea klabu hiyo baada ya kumaliza tofauti na Rais wa Barcelona Joan Laporta ambaye alikuwa kiini cha utata miaka miwili iliyopita.

Messi alikuwa huru mwaka 2021 baada ya mkataba wake kwisha Barca.

Nyota huyo alianza kucheza timu ya wakubwa ya Barcelona mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 16 akicheza michezo 778 na kuwa mchezaji muhimu.

Aliweka rekodi ya mfungaji bora wa Barca akifunga mabao 672 yakiwemo 120 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na rekodi ya mabao 474 La Liga.

Related Articles

Back to top button