Kwingineko

Messi bado mtamu! rekodi zinatisha

MIAMI: Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na mshambuliaji wa Inter Miami, Lionel Messi, anakaribia kufikisha bao lake la 900 katika soka la kulipwa, hatua itakayoongeza rekodi nyingine kubwa katika maisha yake ya soka.

Hii inakuja kufuatia ushindi wa mabao 2-1 walioupata Inter Miami dhidi ya D.C. United katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Marekani.

Tangu ajiunge na klabu hiyo, Messi amecheza michezo 91, akifunga mabao 80 na kutoa pasi 43 zilizosaidia kupata mabao. Hii inamaanisha nyota huyo wa Argentina amehusika moja kwa moja katika jumla ya mabao 123 ndani ya michezo yote aliyocheza.

Katika msimu huu, Messi ameanza kwa kasi baada ya kufunga mabao matatu katika michezo mitatu ya mwanzo ya ligi. Kocha na wachezaji wenzake wamesema mchango wa Messi ni mkubwa na unachangia moja kwa moja mafanikio ya timu.

Mashabiki wa soka duniani sasa wanasubiri kuona kama Messi atafanikisha kufunga bao lake la 900, hatua itakayoongeza rekodi nyingine muhimu katika historia yake ya soka.

 

Related Articles

Back to top button