Kwingineko

Messi aivusha Inter Miami Robo Fainali

FLORIDA:GOLI la pili la penati la dakika za jioni la nahodha na mshambuliaji wa klabu ya Inter Miami, Lionel Messi alilofunga dhidi ya Los Angeles FC (LAFC) limeihakikishia klabu hiyo nafasi ya kucheza katika nusu fainali ya michuano CONCACAF Champions Cup.

Inter Miami imeenda nusu fainali ya michuano hiyo baada ya ushindi wa jumla (aggregate) wa mabao 3-2 baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza kwa bao 1-0 ugenini wiki iliyopita

Los Angeles FC walikuwa wa kwanza kutanua ushindi wao wa jumla dakika ya 9 tu kwa goli la Aaron Long kabla ya Messi kuwafungia kazi na kupachika bao dakika ya 35 na kutoa asisti kwa Noah Allen dakika 61 na ubao kusomeka 2-2 kwenye aggregate

Baadae Inter Miami walipata penati ya maamuzi baada ya kiungo wa LAFC Mark Delgado kuunawa mpira kwenye eneo la 18, penati iliyozaa bao la dakika za jioni na aggregate kusoma 3-2 kisha Miami kufuzu nusu fainali ya nichuano hiyo.

Inter Miami sasa watakutana na Vancouver Whitecaps walioiondosha Pumas FC kwa faida ya goli la ugenini baada ya mchezo wao kumalizika kwa sare ya 3-3 kwenye aggregate.

Related Articles

Back to top button