
LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendeleo kwa michezo mitatu kupigwa Dar es Salaam na Singida huku mechi ya siku ikiwa kati ya Yanga na Mbeya City.
Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 29 baada ya mchezo 11 itakuwa mwenyeji wa Mbeya City katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Yanga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wa ligi msimu wa 2022/23 na inashika rekodi ya kutopoteza michezo 48.
Mbeya City ambayo ililazimisha sare ya bao 1-1 na Simba Novemba 23 ipo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 19 baada ya michezo 13.
Katika mchezo mwingine wa ligi utakaofanyika katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Singida Big Stars itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting.
Singida BS ipo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 21 baada ya michezo 12 wakati Ruvu Shooting inashika nafasi ya 13 ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 13.
Nyasi za uwanja wa Liti mjini Singida zitawaka moto wakati wenyeji Dodoma Jiji itakapoikaribisha Namungo.
Namungo ipo nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi ikiwa na ponti 15 baada ya michezo 12 wakati Dodoma Jiji inashika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 12.