Kwingineko

Mbappé kukabiliwa na hasira za mashabiki

TIMU ya Paris Saint-Germain inaamini Kylian Mbappé anaweza kukabiliwa na chuki inayotokana na hasira za mashabiki wa klabu hiyo msimu ujao asiporekebisha mgogoro wa mkataba wake.

Katika mahojiano na tovuti ya michezo L’Equipe ya Ufaransa mwisho wa wiki fowadi huyo amesema : “PSG ni timu yenye mgawanyiko, klabu yenye mpasuko.”

Mbappé ambaye amekuwa akihusishwa kuhamia Real madrid ameiambia PSG hatasaini mkataba mpya.

Amesema hataondoka majira haya ya joto na badala yake ataondoka akiwa huru wakati mkataba wake wa sasa utakapokwisha mwaka ujao.

Siku za mwisho za Lionel Messi katika klabu ya PSG zilikumbwa na upinzani wa mashabiki baada ya kuwekwa wazi kuwa ataondoka huku klabu ikiongeza ulinzi kwenye makazi yake na pia ya Neymar.

Wiki iliyopita Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi alisema: “Iwapo Kylian Mbappé anataka kubaki, tunataka abaki, ni lazima asaini mkataba mpya. Hatuwezi kumruhusu mchezaji bora duniani kwa sasa aondoka bure.”

Julai 10 Mkurugenzi wa Michezo wa zamani wa PSG Leonardo Nascimento de Araújo amesema ni wakati kwa Mbappé ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa PSG kuondoka.

Related Articles

Back to top button