
MSHAMBULIAJI wa Yanga Fiston Mayele amerejea nchini leo Juni 20 akitokea kwenye kambi ya timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo alicheza mchezo kuitafuta tiketi ya kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika na kufunga moja ya bao katika ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Gabon.
Mayele amewasili mchana wao leo na amekutana na aliyekuwa kocha wa Yanga Nasreddine Nabi ambaye alikuwa akijiandaa kuondoka nchini kwenda kwao Tunisia, wawili hao wamekutana katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julias Nyerere.
Mshambuliaji huyo wa Yanga ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa
“Safari njema Profesa” ameandika Mayele