Mashabiki Yanga, Simba tamasha la utamaduni

Mbio za polepole(jogging) zimefanyika leo mkoani Njombe kuhamasisha wananchi kushiriki Tamasha la Pili la Kitaifa la Utamaduni litakaloanza Agosti 25.
Akizungumza baada ya mbio hizo Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Dkt. Resani Mnata amesema mbio hizo zimehusisha makundi mbalimbali yakiwemo watumishi wa umma, mbio za polepole ya Njombe, polisi, timu ya veteran pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali mjini Njombe.
“Wananchi wanakaribishwa kutumia fursa ya huduma za afya itakayotolewa wakati wote wa tamasha ili waweze kupima bure wa afya zao kwa magonjwa yasiyoambukiza, tutakuwa pia na michezo mbalimbali ikiwemo mechi baina ya washabiki wa timu za Simba na Yanga mkoani humo,” amesema Dkt Mnata.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Agosti 25-27, 2023 katika viwanja vya stendi kuu ya zamani mkoani Njombe.