EPL

Manchester City yakomba mamilioni ya UEFA

MANCHESTER:KLABU ya Manchester City imevuna kiasi cha Euro milioni 5.17, kiwango kikubwa kuliko klabu nyingine yoyote ikiwa kama motisha kutoka shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kwa klabu kwa ajili ya timu kuruhusu wachezaji wao kushiriki michuano mbalimbali ya timu za taifa inayosimamiwa na UEFA.

Jumla ya Euro milioni 233 zimegawanywa kwa timu 901 za wanachama wote 55 wa UEFA kwa kuruhusu wachezaji Kwenda kwenye michuano mbali mbali ya shirikisho hilo kama UEFA Nations League msimu wa 2020/21 na msimu 2022/23, European Championship qualifiers 2022/24 pamoja na michuano ya Euro 2024 iliyofanyika nchini Ujerumani.

Klabu zote zilipokea mgao sawa kwa kila mchezaji iliyomruhusu kwa kila shindano la UEFA Nations League na ile ya kufuzu kwa michuano ya Euro lakini pia kiwango sawa kwa kila mchezaji aliyecheza kwa siku kwenye kila mchuano na klabu zote hata ile ya Daraja la chini kabisa kama Yorkshire Amateur ya England imepokea kiasi cha euro 7300

Rais wa UEFA Aleksander Ceferin amesema klabu zitaendelea kupokea mgao huo kwa mchango wao wa kuendeleza na kuipa msisimko michuano inayohusisha timu za taifa kwa kuruhusu majina makubwa kuwa sehemu ya michuano hiyo.

“Ni jambo jema kuona klabu za ukubwa na viwango vyote kwenye mpira wetu vikipokea zawadi kwa mchango wao wa kuipa msisimko michuano ya timu za taifa ikiwemo ile iliyofanikiwa sana ya UEFA EURO 2024. Tutashea na kila mtu mafanikio ya michuano yetu na huu ni Ushahidi tosha kwa ule msemo wetu wa mpira ukikua kila mtu anafaidika” -amesema Ceferin

Vigogo wengine waliofaidika na mgao huo ni Real Madrid ya Spain iliyolamba euro milioni 4.79 na Inter Milan kutoka Serie A waliopewa euro 4.65

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button