Kwingineko

Manchester City taabani Ligi ya Mabingwa Ulaya

...vipigo vitatu mfululizo

MANCHESTER, England

KLABU ya Manchester City ya England wametolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kipigo cha jumla ya mabao 5-1 kutoka kwa Real Madrid.

City walikubali kipigo cha mabao 3-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu nchini Hispania kabla ya kufungwa mabao 2-1 jana katika Uwanja wa Etihad jijini Manchester , England.

Hiyo ni mara ya tatu mfululizo kwa City kuondolewa na miamba hiyo ya Hispania, hali inayozidi kuweka shinikizo kwa kocha wao Pep Guardiola huku matumaini ya kurejea kwenye makombe yakizidi kufifia.

Katika mchezo wa awali, Federico Valverde aling’ara kwa kufunga hat-trick katika mchezo wa kwanza, huku Vinicius Junior akiongeza mabao mawili na kuondoka na ushindi wa 2-1 katika mchezo wa marudiano uliochezwa Etihad jana, ambapo pia Bernardo Silva alitolewa kwa kadi nyekundu.

Guardiola amesema kuwa hali ilikuwa ngumu kwa timu yake hasa baada ya kucheza pungufu kufuatia kadi nyekundu, lakini bado anaamini kikosi chake kina uwezo na mustakabali mzuri.

“Ni vigumu ukiwa nyuma kwa mabao mengi na unacheza wachezaji 10 dhidi ya 11, lakini tulijitahidi. Tuna kikosi bora na mustakabali mzuri,” Amesema Guardiola.

Sasa macho ya City yako kwenye fainali ya Carabao Cup dhidi ya Arsenal, mchezo unaoweza kuamua mwelekeo wa msimu wao. Kipigo kingine kinaweza kuharibu ndoto zao za taji msimu huu.

Mbali na hilo, City pia wanakabiliwa na ratiba ngumu ikiwemo robo fainali ya FA Cup dhidi ya Liverpool, pamoja na mechi muhimu za Premier League dhidi ya wapinzani wao wakubwa.

Guardiola amekiri kuwa matokeo yao hayajawa mazuri hivi karibuni, lakini anaamini ni suala la muda tu kabla ya timu kurejea kwenye ubora wake.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button