EPLKwingineko
Man UTD yasaka saini ya Neymar

KLABU ya Manchester United imeanzisha mazungumzo na Paris Saint-German(PSG) kuhusu uwezekano wa kumsajili Neymar majira haya ya joto.
Habari kutoka Ufaransa zimesema vilabu kadhaa vya Ligi Kuu England vimefanya majadiliano kuhusu kumsajili mchezaji huyo huku Manchester United ikioonekana kuwa na nia zaidi.
Mapema mwaka huu baadhi ya mashabiki wa PSG walipigwa picha nje ya nyumba nyota huyo wa Brazil wakitaka aondoke klabu hiyo.
Mkataba wa sasa wa Neymar katika timu ya PSG unafika mwisho 2025.
Nyota mwingine wa PSG, Lionel Messi anatarajiwa pia kuondoka msimu huu wakati mkataba wake utakapofika mwisho na hakuna dalili za kuongezewa baada ya hivi karibuni kupewa adhabu kufuatia hatua yake ya kusafiri nje ya klabu bila ruhusa.