
WAKATI joto la dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga likizidi kupanda, makocha wa timu hizo leo wametambaina kushinda katika mechi hiyo Aprili 16.
Mechi hiyo ya Dabi ya Kariakoo yenye mashabiki wengi ndani na nje ya nchi itapigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
“Lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi na kucheza vizuri, nawajua vizuri wapianzani wetu Yanga tunawaheshimu lakini tumejipanga. Mpira kwangu ni sanaa napenda wachezaji wacheze na kuwafurahisha mashabiki pia,” amesema Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira.

Naye Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema timu iko tayari kwa ajili ya mchezo huo.
“Tumejiandaa vizuri na kwa utulivu mkubwa, tunajua kesho tunakwenda kwenye moja kati ya michezo mikubwa Afrika na sio kila mara tunacheza mechi inakuwa na mashabiki zaidi ya elfu hamsini ni lazima tuwatendee haki na tumejiandaa vizuri kwa hilo,” amesema Kaze.
Katika mchezo wa kwanza wa Dabi ya Kariakoo msimu wa 2022/2023 uliopigwa Oktoba 23, 2022 timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.