Nyumbani

Majizo: Sikumchagua Ssebo kwa bahati mbaya

DAR ES SALAAM :MKURUGENZI wa Kituo cha EFM , Francis Siza maarufu kama Mhimili, ameeleza masikitiko yake kufuatia  kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Biashara na Uendeshaji  wa Kituo Cha EFM,  Dennis Busulwa aliyefariki dunia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mtangazaji na DJ wa kituo hicho, Majizzo, ameandika ujumbe wa kugusa hisia akimkumbuka marehemu kama mtu aliyekuwa nguzo muhimu katika ujenzi na maendeleo ya EFM na TVE.

Majizzo ameandika kuwa Ssebo alikuwa mtu aliyepambana kwa nguvu kuhakikisha mafanikio ya taasisi hiyo, huku akisisitiza kuwa mchango wake ulikuwa mkubwa si tu kazini bali pia katika maisha yake binafsi.

“This man standing in front of the EFM logo, ameipambania sana hiyo logo. Alikuwa mhimili muhimu sana kwa EFM na TVE. Silisemi hili leo akiwa amelala, rejea post zangu nyingi kuhusu yeye,” ameandika Majizzo.

Ameongeza kuwa uhusiano wao haukuishia kazini pekee, kwani alimchagua marehemu kuwa msimamizi wa ndoa yake, jambo linaloonesha nafasi kubwa aliyokuwa nayo katika maisha yake.

“Nje ya kazi, mimi kumchagua awe msimamizi wa ndoa yangu haikuwa bahati mbaya; inaeleza alikuwa na maana gani katika maisha yangu binafsi,” ameandika.

Majizzo pia ameeleza kumbukumbu nyingi walizoshirikiana katika safari ya kazi, akisema walifanya vipindi pamoja huku yeye akiwa DJ na marehemu akiwa mtangazaji, wakipitia changamoto na mafanikio katika harakati za kujenga kituo hicho.

“Nakumbuka hustle zote alivyoshiriki kuijenga EFM, kupata na kukosa pamoja, furaha zetu na machozi yetu. Mungu mwenyewe anajua. Nyuma yake, mbele yetu,” ameongeza.

Aidha, Majizzo ametangaza kuwa shughuli za kumuaga marehemu zitafanyika Jumamosi katika viwanja vya Posta, Kijitonyama, ambapo ndugu, jamaa na marafiki watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.

Related Articles

Back to top button