Masumbwi

Majiha kuzichapa na ‘Msauzi’

DAR ES SALAAM: BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Fadhili Majiha anatarajia kutetea mkanda wake wa Ubingwa wa Afrika (WBC) dhidi ya Sabelo Ngebinyana kutoka Afrika Kusini.

Majiha ambaye ana nyota tatu na nusu katika viwango vya boxing rec, atazichapa na Ngebinyana katika pambano la raundi 10, uzito wa kati litakalofanyika  Julai 20 mwaka huu mkoani Mbeya.

Bondia huyo anatetea mkanda huo alioupata Oktoba 28, mwaka jana baada ya kumchapa Bongani Mahlangu kutoka Afrika Kusini.

Akizungumza na Spotileo baada ya kutambulisha pambano hilo, Majiha amesema anatarajia kuondoka kesho kuelekea Malawi kwa ajili ya kuweka kambi na maandalizi mazuri.

Amesema amemfatilia mpinzani wake huyo kuona ubora na madhaifu yake anaimani kwa maandalizi mazuri atafanya vizuri na kutetea mkanda huo.

“Nimejipanga vizuri kutokana na mazoezi ninayofanya kupitia gmy yangu Uwanja wa Kivita chini ya kocha wangu, Kocha Khamis (Kamwe) na ataelekea Malawi kujiandaa vikamilifu.

Ameongeza kuwa anaenda kutetea mkanda huo lakini kuiwakilisha vema bendera ya Tanzania kwa kumpiga mpinzani wake huyo mapema kulingana na mpinzani wake anavyokuja.

Promota wa pambano hilo, Saada Kasonso amesema kutakuwa na mapambano tisa ya utangulizi kwa kuwapa nafasi mabondia vijana ambao hawajaonekana sana ulingoni.

“Pambano lina sura nyingi mpya,ikiwemo vijana wenye  vipaji waliotoka katika pambano la champion wa kitaa lililofanyika mwaka jana,” amesema Saada.

Mapambano ya utangulizi yatakuwa ya Idd Piarali dhidi ya Kiaku Ngoy wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC), Abeid Zugo atapigana dhidi ya  Ayabonga Sonjica  kutoka Afrika Kusini.

Wengine Benjamini Mchukunzi dhidi ya Nicolaus Mode, Daima Bashiru dhidi ya James Kiliani,  Nassibu Habibu atapigana na Abuu Lubanja, Kelvin Ngedere dhidi ya Ajemi Amani, Mubarack Ramadhani dhidi ya George Kandulu na Emmanuel Mwakyembe atazichapa na Gabriel Ochieng wa Ghana.

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button