Majaliwa: Tuiombee Yanga

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuungana kwa pamoja kuiombea timu ya Yanga ili ifanye vizuri katika mchezo wa mkondo wa pili wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa Juni 3, Algeria.
Akizungumza wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu bungeni Jijini Dodoma asubuhi hii Majaliwa amesema ni wakati kwa Watanzania wote kuungana ili kuandika historia kwa pamoja na hana shaka na uwezo wa Yanga.
“Timu yetu ina uwezo mkubwa hivyo tuiombee, niungane na watanzania wenzangu kumshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutoa usafiri kwa Yanga, Mwenyezi Mungu awatangulie ili wakaandike historia,” amesema Majaliwa.
Yanga inaondoka asubuhi hii kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo huo ambapo inahitaji ushindi wenye faida kwao ili kuwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika.