Africa

Ligi ya mabingwa Afrika kutimua vumbi leo

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi inaanza kutimua vumbi leo kwa michezo miwili ya kundi C na D.

Miamba ya soka Afrika Kaskazini klabu ya Raja Casablanca ya Morocco itakuwa mwenyeji wa Vipers ya Uganda kwenye uwanja wa Mohammed V.

Mchezo wa kundi D utashuhudia CR Belouizdad ya Algeria ikiwa mgeni wa El Zamalek ya Misri kwenye uwanja wa Kimataifa wa Cairo.

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo Simba iliyopo kundi C itashuka dimba la 28 Septembre Februari 11 katika mji mkuu wa Guinea, Conakry kuwakabili wenyeji wao, Horoya.

Related Articles

Back to top button