Ligi Mabingwa mikoa wanawake Aprili 29

LIGI ya Mabingwa wa Mikoa Wanawake(WRCL2022) inatarajiwa kuanza Agosti 29 mpaka Septemba 7, 2022 jijini Mwanza.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesema timu zitawasili kwenye kituo Agosti 27, kikao cha maandalizi, droo na ratiba kikifanyika Agosti 28.
“Timu mbili zitakazomaliza nafasi za juu zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza Wanawake(WFDL) msimu wa 2022/2023,” imesema taarifa hiyo ya TFF.
TFF imezitaja timu 20 zilizothibitisha kushiriki kuwa ni JMK Park Queens(Dar es Salaam), Masala Queens(Dar es Salaam), Kinondoni Queens(Dar es Salaam), Coastal Ladies(Tanga), Mt Hanang Queens(Manyara), Udom Queens(Dodoma), Singida Warriors(Singida), Black Mamba(Tabora), Mwanga City Queens(Kigoma) na Geita Gold Queens(Geita).
Nyingine ni Bunda Queens(Mara), Mwanza Star(Mwanza), Mwanya FDC(Shinyanga), Ruangwa Queens)Lindi), Mbinga Queens(Ruvuma), Njombe Queens(Njombe),Ilula FDC(Iringa), Icon Queens(Mbeya), Majimoto Queens(Songwe) na Bende Queens(Rukwa).