Simba ‘oya oya’ Misri
ISMAILIA: SIMBA imeweka wazi mipango ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Fadlu Davis wakiwa nchini humo ni kucheza michezo mitatu ya kirafiki na timu ambazo zitawapa ushindani mkubwa.
Simba ambao wameingia kambi ya maandalizi jana nchini Misri, na kufuatiwa na kocha Fadlu ambaye ameingia nchini humo asubuhi ya leo na jioni hii anatarajia kuanza rasmi ya kukinoa kikosi hicho kwa msimu wa ujao wa Ligi Kuu Bara na kombe la Shirikisho Afrika.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema licha ya timu kuanza mazoezi mepesi jana, baada ya kocha kuwasili nchini humo, leo jioni wanaanza ratiba rasmi ya maandalizi kuelekea msimu msimu mpya wa mashindano.
“Leo kundi la pili limewasili nchini Misri akiwemo na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha wetu Fadlu na kuanza rasmi ratiba ya mazoezi ya msimu mpya, mazoezi yatakuwa mara mbili kwa siku asubuhi na jioni,” amesema Ahmed Ally.
Amesema watafanya mazoezi ya Gym na Uwanjani kwa ajili ya kutafuta utimamu wa mwili wa wachezaji ambao wengi wao wametoka kwenye mapumziko baadae watakuwa na michezo mitatu ya kirafiki.
“Tukiwa nchini humu tutacheza mechi tatu za kirafiki bado timu hazijaweka wazi, kwanza zoezi lililopo kwa kocha wetu anaandaa timu yake, kuwafahamu wachezaji na kuwapa mbinu na ufundi baadae tutacheza mechi hizo,” amesema Meneja huyo.
Wakati huo huo Meneja huyo aliweka wazi suala la utambulisho wa nyota wapya unaendelea lakini leo watakuwa na zoezi la kutoa ‘THANK YOU” kwa wachezaji hawatakuwa sehemu ya timu hiyo.
Nyota ambaye anakutana na THANK YOU ni kiungo mkabaji, Babacar Sarr aliyesajiliwa kipindi cha dirisha dogo pamoja na Pa Omary Jobe naye muda wowote anaweza kukutana na neno hilo na Freddy Michael anayesalia ndani ya timu hiyo iliyopo nchini Misri.