
LIGI Kuu ya soka kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 inaendelea leo kwa michezo minne.
Katika kundi B Yanga itaikabili Dodoma Jiji wakati Polisi Tanzania itaumana na Tanzania Prisons wakati Simba itavaana na Kagera Sugar huku Azam ikikiwasha dhidi ya Ihefu katika kundi D.
Katika michezo ya ufunguzi Juni 21, mabingwa watetezi Mtibwa Sugar imeikandamiza Mbeya City magoli 5-0 huku Ruvu Shooting ikipata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Namungo ikiwa ni mechi za kundi A.
KMC imepoteza kwa magoli 2-0 dhidi ya Geita Gold huku Coastal Union ikipata ushindi mwembamba wa goli 1-0 mbele ya Singida Fountain Gate katika kundi C.
Michezo yote inafanyika kwenye uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, Dar es Salaam.