Leicester yataka saini ya Wout
KLABU ya Leicester City iko katika mazungumzo na timu ya Reims ya Ufaransa kwa ajili ya kumsajili beki wa kibelgiji Wout Faes kuwa mbadala wa Wesley Fofana anayehamia Chelsea’The Blues’.
Fofana anatarajiwa kujiunga na The Blues kabla ya dirisha la uhamisho msimu wa joto kufungwa tarehe Mosi Septemba saa 5 usiku.
Faes mwenye umri wa miaka 24 anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 15 sawa na shilingi bilioni 40.7 na amekuwa na Reims tangu 2020 akiwa amepitia kituo cha kuendeleza vijana cha klabu ya Anderlecht.
Alianza kucheza timu ya taifa ya Ubelgiji akitokea benchi kwenye mchezo wa Ligi ya Mataifa dhidi ya Poland Juni 2022.
Faes amecheza michezo mitatu ya Reims msimu huu na alicheza michezo 37 ya ligi katika timu hiyo msimu uliopita akifunga mabao 4 wakati klabu hiyo ilipomaliza nafasi ya 12 Ligue 1.




