Europa
Kumbe United ilipewa nafasi kumsajili Haaland?

Manchester United ilipewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji mwenye mabao 51 Erling Haaland, 22, kwa £4m alipoichezea Molde ya Norway, mkufunzi wa zamani Ole Gunnar Solskjaer amesema. (The Sun)
United pia wako tayari kuongeza kasi ya kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na Muingereza Declan Rice, 24, lakini Arsenal bado wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili. (The Guardian).
Hata hivyo Ubited wameanza mazungumzo na beki wa Napoli wa Korea Kusini Kim Min-jae. Liverpool na Paris St-Germain pia wanavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Foot Mercato – in French)