World Cup

Kombe la Dunia Wanawake kutimua vumbi leo

MICHUANO ya Fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake inaanza kutimua vumbi leo New Zealand na Australia.

Mwenyeji New Zealand iliyopo Kundi A inaanza kampeni dhidi ya Norway kwenye uwanja wa Eden Park uliopo jiji la Auckland kabla ya Australia kuivaa Ireland katika kundi B kwenye uwanja wa Australia jijini Sydney.

Mataifa ya Afrika yanayoshiriki fainali hizo ni Nigeria, Zambia, Afrika Kusini na Morocco

Michuano hiyo ya Kombe la Dunia kwa wanawake ni ya kwanza kuandaliwa kwa pamoja na nchi mbili.

Kwa mara ya kwanza michuano hiyo inajumuisha mataifa 32 ikiwemo bingwa mtetezi, Marekani.

Makundi ya michuano hiyo ni kama ifuatavyo:

Kundi A
New Zealand, Norway, Philippines, Uswisi

Kundi B
Australia, Canada, Ireland, Nigeria

Kundi C
Costa Rica, Japan, Hispania, Zambia

Kundi D
China, Denmark, England, Haiti

Kundi E
Uholanzi, Ureno, Marekani, Vietnam

Kundi F
Brazil, Ufaransa, Jamaica, Panama

Kundi G
Argentina, Italia, Afrika Kusini, Sweden

Kundi H
Colombia, Ujerumani, Morocco, Korea Kusini

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button