
LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa Dar es Salaam huku mechi kati ya Yanga na KMC ikiwa kivutio.
Yanga ni mwenyeji wa KMC katika uwanja wa Benjamin Mkapa wakati Geita Gold itakuwa mgeni wa Ruvu shooting katika uwanja wa Uhuru.
Yanga inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 6 wakati KMC ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 8.
Katika mchezo wa mwisho wa ligi kati ya timu hizo Mei 19, 2022 Yanga iliifunga KMC mabao 2-0.
Ruvu Shooting na Geita Gold zina pointi 10 na michezo 8 kila moja lakini Ruvu ipo nafasi ya 9 na Geita nafasi ya 10.
Katika mchezo wa mwisho wa ligi kati ya tim hizo Mei 12, 2022 Ruvu Shooting iliibuka mshindi kwa mabao 2-1.