Africa
Kivumbi Simba vs Wydad Ligi ya mabingwa leo

KLABU ya Simba leo inashuka dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuikabili Wydad AC katika mchezo wa kwanza wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo. Mchezo wa marudiano utafanyika Casablanca, Morocco Aprili 28, 2023.
Katika mechi nyingine za robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika leo Al Ahly itakuwa mwenyeji wa Raja Casablanca huku Mamelodi Sundowns ikiwa mgeni wa CR Belouizdad.
Mchezo mmoja wa robo fainali umefanyika Aprili 21 ambapo Esperance ikiwa ugegeni imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JS Kabylie.