Nyumbani
Kivumbi Ligi ya Championship

PATASHIKA ya Ligi ya Championship inaendelea leo kwa michezo mitatu kwenye viwanja tofauti.
Ruvu Shooting itaikaribisha TMA kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma wakati FGA Talents itakuwa mgeni wa Stand United kwenye uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Mkoani Mtwara, wenyeji Mbeya Kwanza wataikaribisha Mbuni kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Kengold inaongoza Ligi ya Championship ikiwa na pointi 50 baada ya michezo 22 wakati Ruvu Shooting inaburuza mkia ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 21.
Katika mechi mbili za ligi hiyo zilizopigwa Februari 15, Biashara United imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania wakati Kengold imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cosmopolitan.