KIUT mabingwa Mpira wa Wavu Dar

DAR ES SALAAM: TIMU za Wanawake na wanaume ya KIUT zimetawazwa kuwa mabingwa wa Ligi ya Mpira wa wavu Mkoa wa Dar Es Salaam baada ya kumaliza michezo yao ya fainali iliyochezwa kwenye viwanja vya Kampala.
Kwa wanawake KIUT ilifanikiwa kuingia fainali baada ya kuiondoa TPA kwa seti 3-1 katika mchezo wa fainali ya Ligi hiyo na bingwa huyo aliondika na kitita Cha shilingi milioni moja,medali na Kombe,huku TPA ikishika nafasi ya pili na kupata zawadi ya shilingi laki tano ,medali na Kombe huku Jeshi stars akipata shilingi 250,000 na medali.
Kwa upande wa wanaume KIUT iliibuka na ushindi wa seti 3-0 dhidi ya High Voltage katika hatua ya fainali hivyo bingwa kaondoka na kitita cha shilingi milioni moja, Kombe na medali, huku High Voltage imeshika nafasi ya pili, ilipata shilingi laki tano, medali na Kombe na TPA ilimalizia nafasi ya tatu ikipata shilingi 250,000 medali na Kombe.
Mabingwa wengine wa Seria B ni IP.Sports ambao wataugana na TPDC, Nyika (wanaume) kwa upande wa wanawake bingwa ni na Chui ,TPDC na Wazo wamepata nafasi ya kupanda kucheza Seria A katika Ligi ya mkoa ya mwaka ujao .
Akizungumza mara baada ya Ligi hiyo kumalizika Rais wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TVF) Mhandisi Magoti Mtani, aliwapongeza mabingwa wa ligi hiyo kwa mwaka huu pamoja wachezaji na kusema malengo yao wanajipanga na ligi ya taifa mwezi ujao.
“Niwashukuru wadhamini waliojitokeza kusaidia na kuendelea kuwaomba wengine waje kwa wingi kusaidia Ligi ya mwakani,”alisema.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa wavu Mkoa wa Dar Es Salaam (DAREVA) Fredy Mshangama, alisema wameweza kufanikiwa asilimia 90 katika Ligi ya mwaka huu.
Alisema kuwa mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la timu ambayo ni chachu ya kuvutia wawekezaji hamasa na ushindani vimekuwa kwa kiasi kubwa.
Kocha wa KIUT Said Issa, amesema kufanya mazoezi kwa bidii na kufuata maelekezo ndio siri ya ushindi wao kwa pande mbili kutwaa ubingwa kwa mwaka huu .
“Kwa wanaume mchezo ulikuwa mgumu kwani mpinzani wetu High Voltage alitufunga mzunguko wa kwanza 3-1 na mzunguko wa pili 3-1 ,hivyo tulirudi kukaa chini kutafakari vitu gani tufanye ili tushinde na tumeweweza kufanikiwa,”alisema.
Mwisho