Nyavu

Fainali mpira wa wavu kurindima jumamosi

DAR ES SALAAM: FAINALI ya Ligi ya Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es Salaam kwa wanawake na wanaume, inatarajiwa kutimua vumbi Jumamosi na Jumapili (Juni 29 na 30 mwaka huu), viwanja wa Kampala University, jijini Dar Es Salaam.

Mabingwa wa mchezo huo kwa wanawake na wanaume watapata fursa ya kupanda daraja kwa msimu ujao na watakaopoteza watacheza best looser atakayepoteza hapo atashuka daraja .

Fainali ya kwanza kwa wanaume itakuwa, kati ya Bandari na TBS kwa wanawake kutakuwa na mchezo kati ya Bandari dhidi ya TAI, mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa Jumamosi ya Juni 29, mwaka huu.

Mchezo wa fainali ya pili kwa wanaume watakutana Jeshi Stars dhidi ya KIUT, kwa timu za wanawake watacheza Jeshi Stars dhidi ya Tanzania prisons mchezo huo utachezwa Juni 30, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es Salaam (DAREVA), Nassoro Sharifu amesema maandalizi yanaendelea vizuri kuelekea mashindano hayo ya kutafuta bingwa kwa upande wa wanawake na wanaume.

Amesema ligi hiyo inafikia ukingoni, bingwa kwa upande wa wanaume na wanawake watapanda kucheza Seria A na watakaopoteza watashuka hadi Seria B kwa msimu ujao na kujipanga upya.

Back to top button